Msajili wa Baraza la Wataalam wa Maabara (The Health Laboratory Practitioners Council) anapenda kuwataangazia Wataalam wote wa Maabara waliokuwa wamesajiliwa; kwa Sheria ya zamani (Health Laboratory; Technologist Council of 1997) kuwa Sheria hii ilifutwa; baada ya kutungwa kwa Sheria Na 22 (The Health Laboratory Practitioners Council) ya mwaka 2007.
Hivyo Baraza linachukuwa nafasi hii, kuufahamisha Umma na kuwatangazia Wataalam wote wa Maabara kuwa; wanapaswa kubadilisha vyeti vya zamani na kupata vyeti vipya kulingana na Sheria iliyotaja hapo juu. Msajili anapenda vile vile, kuwakumbusha Wataalam wote wa Maabara pamoja na wale ambao wanafanya kazi bila kusajiliwa waombe kusajiliwa mapema iwezekanavyo. Baraza linatoa muda wa miezi sita kuanzia tarehe 01.10.2014; kwa Wataalam wa Maabara wa Afya kubadilisha vyeti vya zamani na kupata vyeti vipya.